Pages

Saturday, 10 October 2015

TANGAZO TOKA IDARA YA UCHUMI

BISMLLAH RAHMAN RAHIM
       AL JAMAATUL  MUSLIMINA L AQSWAA
TANGAZO TOKA IDARA YA UCHUMI
KUTOKANA NA KIKAO CHA WANA JUMUIYA WOTE CHA TAREHE  24/08/2015 ,NAMBO  YA FUATAYO YALIJADILIWA NA KUPITISHWA NA WANAJUMUIYA WOTE. AMBAPO YALIKUWA KUWA NA SEHEMU A NA B
 A.NAMNA  NA KANUNI ZA UCHANGIAJI WA MICHANGO  YA JUMUIYA
B.USAJILI MPYA WA WANAJUMUIYA
SEHEMU .A
1.ADA YA JUMUIYA : mwanajumuiya anatakiwa alipe ada miezi mitatu ya mwanzo shilingi 15000 na baadaye shilingi 5000 kwa kila mwezi mpaka kutimiza kile kiwango kilichowekwa  cha shilingi 50000 kwa mwaka.
2.NJIA ZA UCHANGIAJI MICHANGO YA ADA YA JUMUIYA .
Mwanajumuiya anaweza kuchangia ada kupitia mkono kwa mkono (CASH) au kupitia mitandao ya simu ambayo ni :
1.AIRTEL MONEY…….0686-386925
2.TIGO PESA…………….0655-538938
3.MPESA…………………0757-475535
{majina ya akaunti zote ni seif Mketo}
NB.Ada ya jumuiya ikitumwa kupitia mitandao  ya simu ya jumuiya basi taarifa apewe MCHUMI kati ya : 
 1.SEIF MKETHO…………0682-659701
 2.SALUM DAAWA………..0657-117908
3.TAREHE RASMI YA KUANZA KUCHANGIA MICHANGO HIYO YA ADA YA JUMUIYA
Tarehe ni 01/10/2015 kwani ndiyo wakati ambao watu wengi huwa na uwezo ya kipesa hivyo basi ni vyema kuchangia michango hiyo haraka baada ya kupata pesa hizo  ambapo mtu anaruhusiwa kuchangia hata ada yote ya mwaka kama anauwezo huo. Vilevile tar iliyotajwa hapo juu ndiyo mwanza wa kuhesabiwa michango ya ada hata kwa wale walio kwishatoa mwanzoni.
Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na mmoja kati ya wachumi waliotajwa hapo juu ikiwa kuna kipengele kinautata au hakijafahamika vizuri .
SEHEMU. B
-Wanajumuiya waliona kuwa kuna haja ya kufanya tena usajili kwa mara yingine tena ilia kuwapata wanajumuiya wataokuwa tayari kuungana pamoja ili kuhakikisha malengo ya jumuiya yana fikiwa .lengo kuu hapa ni kupata( active members )
Hivyo basi kama ushazipitia na kukubaliana  sifa anazotakiwa kuwanazo mwanajumuya ambazo zinapatikana katika e-mail ya jumuiya (jumuiyayetu11@gmail.com) password  yetu ni BUKHAR111.Basi unaweza kuthibitisha uwepo wako kwa kuandika jina lako kamili au jina maarufu, na kuandika neno NDIYO au HAPANA.  Au ujumbe mfupi (sms) kwenye no hizi ;
0659-320365 au 0782-477319(Katibu mkuu wa jumuiya SULEIMANI  JUMA).
Tangazo hili limetolea na idara ya uchumi
Wabilah tawfiq.

KALENDA NA SIFA ZA MWANAJUMUIYA



BISMILLAH RAHMANI RAHIM
     JAMAATUL  MUSLIMIN AL AQSWAA
KALENDA YA MWAKA YA JUMUIYA .
1.Wanajumuiya lazima wakutane mara moja (1) kwa mwaka  yaani katika likizo ya mafunzo kwa vitendo( Field)
2.viongozi watakutana mara moja (1) kwa mwaka siku mojsa kabla ya kukutana na wanajumuiya wote.
3.viongozi watakutana kuzungumza maswala mbalimbali ya kiutendaji kila baada ya miezi miwili (2)
4.wanajummuiya ni lazima kuangalia taarifa mpya za jumuiya kila baada ya swala ya ijumaa ili kujua nini kimejiri ndani ya jumuiya .
5.wanajumuiya waliokaribu karibu  watakutana kila baada ya miezi mwili .
SIFA ZA MWANAJUMUIYA
1.Awe muislamu ambaye yuko tayari kutimiza malengo yote ya jumuiya
2.Awe na maadilid ya kiislamu na asiwe mfanya makoasa ya dhahiri
3.Awe tayari kusoma dini kadri ya uwezo wake
4.Mwanajumuiya anatakiwa alipe ada ya jumuiya ndani ya miezi mitatu(3) vinginevyo atakuwa amejitoa uwanajumuiya
5.mwanajumuiya anaweza kukopa katika jumuiya ila kwa kufuata  na kuzingatia vigezo na masharti ya mkopo huo
6.Mwanajumuiya ni lazima ashiriki vikao na shughuli zote zinazohusiana na jumuiya
7.Mwanajumuiya  awe tayari kutii viongozi
8.Mwanajumuiya ana uhuru wa kutoka (kujivua uwanajumuiya) kama ataona hakuna umuhimu wa kubaki kama mwanajumuiya


WABILLAH TAWFIQ.

Tuesday, 2 June 2015

Taarifa ya kufunguliwa kwa akaunti za jumuiya kwa ajili ya michango yetu ya kila mwezi pamoja na mchango mingineyo
>>TIGO PESA - 0665538938
>>AIRTEL MONEY- 0686386925
>>M-PESA-0757475537
..........Jina la akaunti zote SEIF MOH'D MKETO..............

TAARIFA FUPI YA JUMUIYA

 

 

3. MAJINA YA VIONGOZI
1. AMIRI …………………………………………………………..MWAPASHUA FUJO
2.KATIBU MKUU………………………………………………….SELEMANI JUMA MZEE
3.NAIBU KATIBU MKUU……………………………………….ABDALLAH SAIDI CHABAI
4AMIRI.ID………………………………………………………SEIF MOHAMEDI MKETO
5.KATIBU IDARA YA FEDHA.………………………………….SALUMU SEIF SHABANI
6.AMIRI IDARA YA HABARI……………………………….SHABANI MZENGA

4. E-MAIL YA JUMUIYA
1. Jumuiyayetu11@gmail.com (neno la siri ni BUKHAR11).Hii ni kwa matumizi ya wanajumuiya wote ,kwa ajili ya maswala yanayohusu jumuiya tu, kama vile taarifa mbalimbali , maoni, ushauri pamoja na uwasilishaji wa mada mbalimbali zinazohusu dini yetu .


5. UENDESHAJI WA JUMUIYA.

Uendeshaji wa jumuiya utategemea sana michangao ya wanjumuiya katika kuendesha shughuli zake mpaka pale tutakapo jaaliwa rasmi  kuanzisha miradi au  biashara itakyobuniwa kwa ajilai ya kuendesha jumuiya yetu .
Hivyo pendekezo lililotolewa katika kuchangia jumuiya kwa kila mwezi ni kiasi cha shilingi 4125/=,kiasi ambacho ni sawa na shilingi 50000/= kwa mwaka mzima ,ambayo itatumika katika shughuli mbalimbali za kuendesha jumuiya yetu.

6. MALENGO YA JUMUIYA HII 
Jumuiya yetu ina malengo ya muda mrefu na malengo ya muda mfupi naya ni kama yafuatayo:-
(i)KUWAHUDUMIA MAYATIMA
Lengo kuu hapa ni kuwasaidi matima katika maswala yanato husu elimu ,chakula pamoja namalezi kwa ujumla ( maadili ya kiislamu) kadri ALLAH SW atakapo tuwezesha ,ili baadaye nao wautumikie uislamu.

ii) KUTOA MSAADA KWA JAMII
Jamii inatakiwa kusaidiwa kwa hali na mali ,hivyo sisi kama waislamu tunajukumu la kusaidia jamii ya kiislamu ingawa na sisi ni wahitaji wa hayo tunayoyatoa kwa wenzetu na wala sisi si matajiri au watu wenye kipato kikubwa .

iii) KUWAANDAA VIJANA KABLA HAWAJAFIKA VYUONI
Ni jukumu la kila muislamu ,kama ni mwalimu ,daktari ,fundi ,mwanahabari ,aumfanya biashara .K ujitahidi kuwaandaa vijana wa kislamu katika shule mbalimbali ,madrasa zetu magerezani pia na hata katika mitaa yetu ili waweze kijitambua kwaajili ya kuutumikia aislamu

iv).KUTAFUTA ARDHI KWA AJILI YA MATUMIZI YA JUMUIYA
Ardhi ni jambo muhimu kwa ulimwengu wa hivi leo kwasababu shughuli nyingi hutegemea ardhi ,kama vile kilimo,biashara ,vituo vya yatima, kujenga misikiti, shule pamoja na kuendesha miradi mbalimbali ya jumuiya.hivyo basi ni jukumu letu kutafuta ardhi kwa shughuli hizo.

 B.KWETU WENYEWE


V) KUFAHAMIANA NA KUJUWANA
Tunatakiwa kufahamian na kutambuana nje na ndani ili kuweza kusaidina katika hali na mali katika majambo mbalimbali na sio siku za harusi tu .vile vile kukutana wajumbe wote lau kwa mwaka mara moja ili kuongeza mahaba na kujadilia mambo yetu kwa pamoja .



VI) KUFAHAMU DINI YETU
Hii hususani inahusu elimu kwa sisi wenyewe tusome na kufanyia kazi yake tunayoyasoma ,kwa maana hiyo tujiwekee utaratibu wa kuuandaa mada mbalimbali zinazohusu dini na kuziwasilisha kwa manajumuiya kupitia e-mail ya jumuiya kwa madhumuni ya kupata walau elimu itakayotufaa katika maisha ya hapa duniani na kesho akhera


VII) KUTEKELEZA A’MALI MBALIMBALI KWA AJILI YA ALLAH
Tuwe na mipango ya kupaga kila muda kuongeza utekelezaji wa a’amali kwa ajili ya akhera yetu na dunia yrtu .Kama vile tujiwekee mipango ya muda mfupi na muda mrefu kama vile swala za usiku ,kumdhukuru Allah ,na kumswalia Mtume (s. a.w) ,amoja na kufanya istighifari na kujiweka mbali na kufanya maasi. Vilevile kuweka mikalati yamuda mrefu kama vile kwenda hija  pale Allah sw akituwezesha .


VII) HITIMISHO.
mlango wa maoni yako wewe mjumbe wa  jumuiya yetu haujafungwa hivya basi onaombwa utoe maoini yako kwa ajilia ya ya kujenga na kuendeleza jumuiya yetu , hivyo ni jukum la kila mtu kutoa maoni yake mwanzo wa  taarifa. Ni vyema tushirikiane kwa pamoja kwasababu jumuiya hii si ya watu Fulani bali ni ya  wanajumuiya wote  ni lazima mawazo ya mtu yaheshimiwe  na kama yatakubalika ni lazima yafanyiwe kazi kwa maendeleo ya jumuiya. Inshaallah sw atulipe kila la kheri . na atujaalie tuwe wnye kutekeleza na kuyasimamia yale tuliyoyakusudia kuyafanya kwa uwezo wake Allah sw.

WABILLAH TAWFIQ.
 

For more contacts visit:-

http://www.jumuiyayetu.blogspot.com