Tuesday, 2 June 2015

TAARIFA FUPI YA JUMUIYA

 

 

3. MAJINA YA VIONGOZI
1. AMIRI …………………………………………………………..MWAPASHUA FUJO
2.KATIBU MKUU………………………………………………….SELEMANI JUMA MZEE
3.NAIBU KATIBU MKUU……………………………………….ABDALLAH SAIDI CHABAI
4AMIRI.ID………………………………………………………SEIF MOHAMEDI MKETO
5.KATIBU IDARA YA FEDHA.………………………………….SALUMU SEIF SHABANI
6.AMIRI IDARA YA HABARI……………………………….SHABANI MZENGA

4. E-MAIL YA JUMUIYA
1. Jumuiyayetu11@gmail.com (neno la siri ni BUKHAR11).Hii ni kwa matumizi ya wanajumuiya wote ,kwa ajili ya maswala yanayohusu jumuiya tu, kama vile taarifa mbalimbali , maoni, ushauri pamoja na uwasilishaji wa mada mbalimbali zinazohusu dini yetu .


5. UENDESHAJI WA JUMUIYA.

Uendeshaji wa jumuiya utategemea sana michangao ya wanjumuiya katika kuendesha shughuli zake mpaka pale tutakapo jaaliwa rasmi  kuanzisha miradi au  biashara itakyobuniwa kwa ajilai ya kuendesha jumuiya yetu .
Hivyo pendekezo lililotolewa katika kuchangia jumuiya kwa kila mwezi ni kiasi cha shilingi 4125/=,kiasi ambacho ni sawa na shilingi 50000/= kwa mwaka mzima ,ambayo itatumika katika shughuli mbalimbali za kuendesha jumuiya yetu.

6. MALENGO YA JUMUIYA HII 
Jumuiya yetu ina malengo ya muda mrefu na malengo ya muda mfupi naya ni kama yafuatayo:-
(i)KUWAHUDUMIA MAYATIMA
Lengo kuu hapa ni kuwasaidi matima katika maswala yanato husu elimu ,chakula pamoja namalezi kwa ujumla ( maadili ya kiislamu) kadri ALLAH SW atakapo tuwezesha ,ili baadaye nao wautumikie uislamu.

ii) KUTOA MSAADA KWA JAMII
Jamii inatakiwa kusaidiwa kwa hali na mali ,hivyo sisi kama waislamu tunajukumu la kusaidia jamii ya kiislamu ingawa na sisi ni wahitaji wa hayo tunayoyatoa kwa wenzetu na wala sisi si matajiri au watu wenye kipato kikubwa .

iii) KUWAANDAA VIJANA KABLA HAWAJAFIKA VYUONI
Ni jukumu la kila muislamu ,kama ni mwalimu ,daktari ,fundi ,mwanahabari ,aumfanya biashara .K ujitahidi kuwaandaa vijana wa kislamu katika shule mbalimbali ,madrasa zetu magerezani pia na hata katika mitaa yetu ili waweze kijitambua kwaajili ya kuutumikia aislamu

iv).KUTAFUTA ARDHI KWA AJILI YA MATUMIZI YA JUMUIYA
Ardhi ni jambo muhimu kwa ulimwengu wa hivi leo kwasababu shughuli nyingi hutegemea ardhi ,kama vile kilimo,biashara ,vituo vya yatima, kujenga misikiti, shule pamoja na kuendesha miradi mbalimbali ya jumuiya.hivyo basi ni jukumu letu kutafuta ardhi kwa shughuli hizo.

 B.KWETU WENYEWE


V) KUFAHAMIANA NA KUJUWANA
Tunatakiwa kufahamian na kutambuana nje na ndani ili kuweza kusaidina katika hali na mali katika majambo mbalimbali na sio siku za harusi tu .vile vile kukutana wajumbe wote lau kwa mwaka mara moja ili kuongeza mahaba na kujadilia mambo yetu kwa pamoja .



VI) KUFAHAMU DINI YETU
Hii hususani inahusu elimu kwa sisi wenyewe tusome na kufanyia kazi yake tunayoyasoma ,kwa maana hiyo tujiwekee utaratibu wa kuuandaa mada mbalimbali zinazohusu dini na kuziwasilisha kwa manajumuiya kupitia e-mail ya jumuiya kwa madhumuni ya kupata walau elimu itakayotufaa katika maisha ya hapa duniani na kesho akhera


VII) KUTEKELEZA A’MALI MBALIMBALI KWA AJILI YA ALLAH
Tuwe na mipango ya kupaga kila muda kuongeza utekelezaji wa a’amali kwa ajili ya akhera yetu na dunia yrtu .Kama vile tujiwekee mipango ya muda mfupi na muda mrefu kama vile swala za usiku ,kumdhukuru Allah ,na kumswalia Mtume (s. a.w) ,amoja na kufanya istighifari na kujiweka mbali na kufanya maasi. Vilevile kuweka mikalati yamuda mrefu kama vile kwenda hija  pale Allah sw akituwezesha .


VII) HITIMISHO.
mlango wa maoni yako wewe mjumbe wa  jumuiya yetu haujafungwa hivya basi onaombwa utoe maoini yako kwa ajilia ya ya kujenga na kuendeleza jumuiya yetu , hivyo ni jukum la kila mtu kutoa maoni yake mwanzo wa  taarifa. Ni vyema tushirikiane kwa pamoja kwasababu jumuiya hii si ya watu Fulani bali ni ya  wanajumuiya wote  ni lazima mawazo ya mtu yaheshimiwe  na kama yatakubalika ni lazima yafanyiwe kazi kwa maendeleo ya jumuiya. Inshaallah sw atulipe kila la kheri . na atujaalie tuwe wnye kutekeleza na kuyasimamia yale tuliyoyakusudia kuyafanya kwa uwezo wake Allah sw.

WABILLAH TAWFIQ.
 

For more contacts visit:-

http://www.jumuiyayetu.blogspot.com

No comments:

Post a Comment