VITABU VYA DINI

al-´Ibrah fiy Shahr-is-Swawm
´Abdul-´Muhsin al-´Abbaad

www.wanachuoni.com

al-´Ibrah fiy Shahr-is-Swawm

Mazingatio katika mwezi wa funga

Mwandishi: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad al-Badr
Mfasiri: Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush
al-´Ibrah fiy Shahr-is-Swawm
´Abdul-´Muhsin al-´Abbaad
2
www.wanachuoni.com
Dunia ni nyumba ya majaribio na mtihani .......................................................................... 3
Msimu katika misimu ya Aakhirah ...................................................................................... 5
Kuzidisha kheri ........................................................................................................................ 6
Kutoka kheri kwenda nyingine ............................................................................................. 7
Mazingatio katika mwezi wa Swawm ................................................................................. 9
Ya kwanza ........................................................................................................................... 10
Ya pili .................................................................................................................................. 12
Ya tatu ................................................................................................................................. 13
Ya nne ................................................................................................................................. 14
Hitimisho ............................................................................................................................... 20
al-´Ibrah fiy Shahr-is-Swawm
´Abdul-´Muhsin al-´Abbaad
3
www.wanachuoni.com
Dunia ni nyumba ya majaribio na mtihani Dunia ni nyumba ya majaribio na mtihani Dunia ni nyumba ya majaribio na mtihani Dunia ni nyumba ya majaribio na mtihani Dunia ni nyumba ya majaribio na mtihaniDunia ni nyumba ya majaribio na mtihani Dunia ni nyumba ya majaribio na mtihani Dunia ni nyumba ya majaribio na mtihani Dunia ni nyumba ya majaribio na mtihaniDunia ni nyumba ya majaribio na mtihani Dunia ni nyumba ya majaribio na mtihani Dunia ni nyumba ya majaribio na mtihani Dunia ni nyumba ya majaribio na mtihani Dunia ni nyumba ya majaribio na mtihani Dunia ni nyumba ya majaribio na mtihani Dunia ni nyumba ya majaribio na mtihaniDunia ni nyumba ya majaribio na mtihaniDunia ni nyumba ya majaribio na mtihani Dunia ni nyumba ya majaribio na mtihani
Allaah Ameumba viumbe Wake ili wamwabudu Yeye Mmoja asiyekuwa na mshirika. Amesema katika Kitabu Chake Titukufu: وَمَا خَلَقْتُ الِْْنَّ وَالِْْنسَ إِلََّّ لِيَ عْبُدُونِ
“Na Sikuumba majini na wanadamu wa isipokuwa waniabudu.”1
Ametuma Mitume Wake watukufu ili wawaoneshe waja njia ya ´ibaadah: وَلَقَدْ ب عََثْ نَا فِِ كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُوالَّ أَنِ اعْبُدُوا اللَّ هَ واجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ
“Na kwa yakini Tulituma katika kila ummah Rasuli (awaamrishe watu wake) kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na twaaghuwt (miungu ya uongo).”2
Amefanya maisha ya dunia kuwa ni sehemu ya majaribio yao na mtihani ili waoneshe ni nani katika wao alie na matendo mazuri: الَّذِي خَلَقَ الْمَوْتَ وَالَْْيَاةَ لِيَبْ لُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَال
“Ambaye Ameumba mauti na uhai ili Akujaribuni ni nani kati yenu mwenye ‘amali nzuri zaidi.”3
Kisha Akasema: وَهُوَ الْعَزِيزُ الْغَفُ ورُ
“Naye ni Al- ‘Aziyzul-Ghafuwr (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwingi wa kusamehe).”4
1 51:56
2 16:36
3 67:02
4 67:02
al-´Ibrah fiy Shahr-is-Swawm
´Abdul-´Muhsin al-´Abbaad
4
www.wanachuoni.com
Amesema hivi ili kuonesha kuwa Anawalipa hawa wanaopewa mtihani wanaotenda matendo mema. Malipo haya yametokamana na Jina Lake al-Ghafuur (Mwingi wa kusamehe). Upande mwingine Ameonesha pia kuwa wale wasiotenda matendo mazuri wanastahiki kuadhibiwa kutokana na Jina Lake al-´Aziyz (Mwenye enzi ya nguvu asiyeshindika daima). Hili linaenda sambamba na Kauli Yake: وَأَنَّ عَذَابِِ هُوَ الْعَذَابُ الَْْلِيمُ
5“Na kwamba Adhabu Yangu, ndiyo adhabu iumizayo.”
5 15:50
al-´Ibrah fiy Shahr-is-Swawm
´Abdul-´Muhsin al-´Abbaad
5
www.wanachuoni.com
Msimu katika misimu ya Aakhirah Msimu katika misimu ya Aakhirah Msimu katika misimu ya Aakhirah Msimu katika misimu ya Aakhirah Msimu katika misimu ya Aakhirah Msimu katika misimu ya Aakhirah Msimu katika misimu ya Aakhirah Msimu katika misimu ya Aakhirah Msimu katika misimu ya Aakhirah Msimu katika misimu ya Aakhirah Msimu katika misimu ya Aakhirah Msimu katika misimu ya Aakhirah Msimu katika misimu ya Aakhirah Msimu katika misimu ya Aakhirah Msimu katika misimu ya Aakhirah
Kama jinsi Allaah Amevyofadhilisha baadhi ya watu juu ya wengine na baadhi ya sehemu juu ya zingine, kadhalika Amefadhilisha baadhi ya zama kuliko zingine. Miongoni mwa hayo Amefadhilisha mwezi wa Ramadhaan uliobarikiwa kuliko miezi mingine. Ameutofautisha na miezi mingine na Kuuchagua kuwa ni mwezi wa wajibu kwa watu kufunga: وَرَبُّكَ يََْلُقُ مَا يَشَاءُ وَيََْتَارُ
“Na Mola wako Anaumba Atakavyo, na Anachagua (Atakavyo).”6
Allaah Ameufadhilisha mwezi huu na Kuufanya kuwa ni msimu bora. Humo wanashindishana waja katika kumwabu Allaah ili waweze kufikia mafanikio na kujikurubisha kwa Allaah. Wanajikurubisha kwa Mola Wao kwa kufunga mchana na kusimama usiku na kusoma Kitabu Chake Kitukufu ambacho haitokifikia ubatili mbele yake na wala nyuma yake; ni uteremsho kutoka kwa Mwenye hikmah wa yote daima na Mwenye kustahiki kuhimidiwa. Wanajikurubisha kwa Allaah kupitia hicho na utiifu mwingine wote. Lakini wakati huo huo wanapofanya hayo, wanajitenga na kujiweka mbali na maasi na madhambi: ي رَْجُونَ تَِِارَةا لَّن تَ بُورَ لِيُ وَفِّ يَ هُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ إِۚنَّهُ غَفُورٌ شَكُورٌ
“Wanataraji tijara isiyofilisika. Ili (Allaah) Awalipe ujira wao timilifu na Awazidishie kutokana na fadhila Zake. Hakika Yeye ni Ghafuwrun-Shakuwr (Mwingi wa kusamehe - Mwingi wa kupokea shukurani).”7
6 28:68
7 35:29-30
al-´Ibrah fiy Shahr-is-Swawm
´Abdul-´Muhsin al-´Abbaad
6
www.wanachuoni.com
Kuzidisha kheriKuzidisha kheriKuzidisha kheri Kuzidisha kheriKuzidisha kheriKuzidisha kheri Kuzidisha kheriKuzidisha kheri Kuzidisha kheri
Baada ya Allaah Kufaradhisha kufunga Ramadhaan, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawashaji´isha kuifuatisha Ramadhaan kwa kufunga siku zile za Shawwaal. Amefanya hivi ili ujira wao uweze kuwa mkubwa na ili waweze kulipwa kama aliyefunga mwaka mzima. Abu Ayyuub al-Answaariy (Radhiya Allaahu ´anhu) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Anayefunga Ramadhaan na akaifuatisha kwa kufunga siku sita za Shawwaal, ni kama amefunga mwaka mzima.”
Haafidhw al-Mundhiriy amesema:
“Ameipokea Muslim, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa´iy, Ibn Maajah na at-Twabaraaniy amezidisha na kusema: “Nilisema: “Kila siku hulipwa kwa kumi.” Akasema: “Ndio.” Wamepokezi wake ni wapokezi sahihi.
Mwaka hauwezi kuzidi siku 360. Siku sita za Shawwaal zikiwekwa katika Ramadhaan nzima na kila siku moja inalipwa kwa thawabu kumi (kwa kuwa tendo moja zuri linalipwa mara kumi) Waislamu wanazingatiwa kuwa wamefunga mwaka mzima. Kwa ajili hiyo amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Ni kama amefunga mwaka mzima.”
Hiyo ni fadhila kutoka kwa Allaah. Himdi na shukurani zote ni za Allaah zisizohesabika.
al-´Ibrah fiy Shahr-is-Swawm
´Abdul-´Muhsin al-´Abbaad
7
www.wanachuoni.com
Kutoka kheri kwenda nyingineKutoka kheri kwenda nyingineKutoka kheri kwenda nyingineKutoka kheri kwenda nyingine Kutoka kheri kwenda nyingine Kutoka kheri kwenda nyingine Kutoka kheri kwenda nyingine Kutoka kheri kwenda nyingineKutoka kheri kwenda nyingine Kutoka kheri kwenda nyingineKutoka kheri kwenda nyingine Kutoka kheri kwenda nyingine Kutoka kheri kwenda nyingine Kutoka kheri kwenda nyingineKutoka kheri kwenda nyingine
Katika fadhila za Allaah kwa waja Wake ni kwamba Amewasahilishia njia ambazo zinawanyanyua katika daraja. Vile vile Amewajaalia daima mafungamano yenye nguvu na ´ibaadah za Allaah. Baada ya masiku na usiku za Ramadhaan (ambapo ndani yake Allaah Anayasamehe madhambi, Anazinyanyua daraja na kuyafuta makosa) kuisha, viumbe wanakuwa wamemkurubia Mola Wao. Baada ya hapo kidogo huanza miezi ya Hajj, ambapo ndani yake inaendewa Nyumba Tukufu ya Allaah. Siku ya ´Iyd-ul-Fitwr, ambayo ni ile siku ya kwanza ya Shawwaal, ndio siku ya kwanza ya miezi ya Hajj. Allaah (Ta´ala) Amesema juu yake: الَْْجُّ أَشْهُرٌ مَّعْلُومَاتٌ فَۚمَن فَ رَضَ فِيهِنَّ الَْْجَّ فَلَ رَفَثَ وَلََّ فُسُوقَ وَلََّ جِدَالَ فِِ الَْْجِّ وَۚمَا تَ فْعَلُوا
مِنْ خَيٍْْ ي عَْلَمْهُ اللَّ ه وَۚتَ زَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْ رَ الزَّادِ التَّ قْوَ ى وَۚاتَّ قُونِ يَا أُولِِ الَْْلْ بَابِ
“Hajj ni miezi maalumu. Na atakayekusudia kuhiji, basi asifanye tendo la ndoa wala ufasiki wala mabishano katika Hajj. Na lolote mlifanyalo katika ya kheri Allaah Analijua. Na jitengenezeeni akiba. Na hakika bora ya akiba ni taqwa. Na nicheni Mimi enyi wenye akili!”8
Katika Ramadhaan ndio kumeteremshwa Qur-aan iliyobarikiwa. Katika Ramadhaan milango ya Pepo inafunguliwa na milango ya Moto inafungwa. Katika siku za Swawm Mashaytwaan wanafungwa. Allaah (Ta´ala) Amesema kuhusu siku hizi katika Hadiyth al-Qudsiy:
“Kila ´amali ya mwanaadamu inalipwa mara kumi. Isipokuwa Swawm tu. Ni Yangu na Mimi ndio nitailipa.”
Wakati masiku haya hayanaisha, kunakuja masiku ya Hajj. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu masiku haya:
8 02:197
al-´Ibrah fiy Shahr-is-Swawm
´Abdul-´Muhsin al-´Abbaad
8
www.wanachuoni.com
“Atakayefanya Hajj, kisha asiseme maneno machafu wala asitende vitendo vichafu, atarudi akiwa kama siku aliyozaliwa na mama yake.”
Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim na wengine.
Amesema pia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“'Umrah hadi 'Umrah ni kafara [kufutiwa dhambi] baina yao, wakati Hajj iliyokubaliwa haina jazaa isipokuwa ni Pepo.”
Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim na wengine.
Muislamu hakaribii kukamilisha mmoja katika misimu ya Aakhirah, isipokuwa unakuja mwingine mpya. Hili linaendelea ili awe kila siku ni mwenye kumwabudu Mola Wake Aliyemuumba baada ya kukosekana na Akamjazia neema Zake za dhahiri na zilizojificha.
al-´Ibrah fiy Shahr-is-Swawm
´Abdul-´Muhsin al-´Abbaad
9
www.wanachuoni.com
Mazingatio katika mwezi wa SwawmMazingatio katika mwezi wa SwawmMazingatio katika mwezi wa Swawm Mazingatio katika mwezi wa Swawm Mazingatio katika mwezi wa SwawmMazingatio katika mwezi wa SwawmMazingatio katika mwezi wa Swawm Mazingatio katika mwezi wa Swawm Mazingatio katika mwezi wa SwawmMazingatio katika mwezi wa Swawm Mazingatio katika mwezi wa Swawm Mazingatio katika mwezi wa SwawmMazingatio katika mwezi wa SwawmMazingatio katika mwezi wa SwawmMazingatio katika mwezi wa Swawm Mazingatio katika mwezi wa Swawm Mazingatio katika mwezi wa Swawm Mazingatio katika mwezi wa SwawmMazingatio katika mwezi wa SwawmMazingatio katika mwezi wa SwawmMazingatio katika mwezi wa Swawm
Mwezi huu ni mwezi uliyobarikiwa, ambao ni msimu bora miongoni mwa misimu, umeaga Ummah wa Kiislamu siku za karibuni zilizopita. Bishara njema ya Pepo kwa yule ambaye amewafikishwa na Allaah kutenda matendo mema na yakakubaliwa. Khasara kwa yule aliyepitikiwa na masiku haya bila ya kupata tendo lolote jema siku ya Qiyaamah. Ni msiba mkubwa ulioje ikiwa alijishughulisha katika masiku haya katika kumridhisha Shaytwaan na akawa bega kwa bega na matamanio ya nafsi inayoamrisha maovu? Kinga inaombwa kwa Allaah!
Mwezi huu mkubwa una manufaa mengi. Una mazingatio na mawaidha mengi yanayoipa nafsi mapenzi ya kheri na kudumu kwa kumwabudu Allaah. Upande mwingine unaipa nafsi chuki dhidi ya maasi yote na umbali kwa yote yanayomkasirikisha Allaah (´Azza wa Jalla).
Ninajaribu kutaja baadhi ya mazingatio hayo na mawaidha ambayo Muislamu hutoka nayo katika mwezi wa Ramadhaan na ikawa ni kama ukumbusho mzuri kwake mnamo masiku haya yaliyobarikiwa.
Hivyo ninasema ilihali ni mwenye kumuomba Allaah mafanikio:
al-´Ibrah fiy Shahr-is-Swawm
´Abdul-´Muhsin al-´Abbaad
10
www.wanachuoni.com
Ya kwanza
Masiku ya mwezi wa Ramadhaan ni moja kati ya fursa nzuri kwa Waislamu. Pengine yakarudi mara nyingine au zaidi. Pengine yakarudi mauti yakawahi kumchukua. Ni muhimu fursa hii itumiwe kwa kujishughulisha na utiifu na ´ibaadah na kujitenga na madhambi. Jambo ambalo ni muhimu zaidi ya hilo, ni mtu adumu siku zote katika hayo. Katika thawabu za matendo mema ni kwamba yanafuatiwa na matendo mengine mema, kama jinsi madhambi yanaadhibiwa yakifuatiwa na madhambi mengine. Muislamu mwenye kuinasihi nafsi yake anapofikia mwezi huu uliyobarikiwa, hujishughulisha na kumwabudu Mola Wake ambaye Amemuumba ili Amwabudu na Akamjazia neema Zake za dhahiri na zilizojificha. Katika hali hii nafsi yake inaburudika na matendo mema. Katika hali hii moyo wake unatamani Aakhirah, ambayo ndio maisha ya milele na ya mwisho. Siku ambayo mtu atanufaika tu na yale yaliyotangulizwa na mikono yake: ي وَْمَ لََّ يَنفَعُ مَالٌ وَلََّ ب نَُونَ إِلََّّ مَنْ أَتَى اللَّ هَ بِقَلْبٍ سَلِيم
“Siku (ambayo) hayatofaa mali wa watoto. “Isipokuwa yule atakayefika (kwa) Allaah na moyo uliosalimika (kutokana na shirki, kufuru, dhambi, unafiki, uhasidi, chuki, n.k.).”9
Nafsi ikijizoweza utiifu katika masiku haya yaliyobarikiwa kwa kutarajia kupata thawabu kutoka kwa Allaah na kujiepusha na maasi, kwa kukhofia adhabu ya Allaah, inanufaika na utiifu huko mbeleni na kujiepusha na madhambi. Allaah Anatakiwa kuabudiwa kila siku na mja mpaka wakati wa mauti: وَاعْبُدْ رَبَّكَ حَ تَّ يَأْتِيَكَ الْيَقِيُ
“Na mwabudu Mola wako mpaka ikufikie yakini (mauti).”10
9 26:88-89
10 15:99
al-´Ibrah fiy Shahr-is-Swawm
´Abdul-´Muhsin al-´Abbaad
11
www.wanachuoni.com
يَا أَي هَُّا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّ قُوا اللَّ هَ حَقَّ ت قَُاتِهِ وَلََّ تََُوتُنَّ إِلََّّ وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ
“Enyi mlioamini! Mcheni Allaah kama apasavyo kuogopwa na wala msife isipokuwa na nyinyi ni Waislamu.”11
Haimstahikii na wala haijuzu kwa Muislamu ambaye kishapata kuonja ladha ya utiifu katika mwezi wa Swawm, kuweka mahala pa ladha hiyo madhambi. Baada ya kumuudhi adui yake katika mwezi wa Ramadhaan, haijuzu kwake kumfurahisha katika Shawwaal au miezi mingine. Vile vile sio katika sifa za Muislamu mwenye kuinasihi nafsi yake kuyaaga matendo ya kheri na mwezi wa Ramadhaan, kuyabadili kwa mabaya. Mwabudiwa katika Ramadhaan na miezi mingine yote ni mwenye Kueshi na hafi na halali. Kwake yanapandishwa matendo ya mchana kabla ya matendo ya usiku na matendo ya usiku kabla ya matendo ya mchana: وَإِن تَكُ حَسَنَةا يُضَاعِفْهَا وَي ؤُْتِ مِن لَّدُنْهُ أَجْارا عَظِي ا ما
“Na ikiwa ni ‘amali njema Huizidisha na Hutoa kutoka Kwake ujira mkuu.”12
11 03:102
12 04:40
al-´Ibrah fiy Shahr-is-Swawm
´Abdul-´Muhsin al-´Abbaad
12
www.wanachuoni.com
Ya pili
Swawm ni siri baina ya mja na Mola Wake. Hakuna mwingine anayejua uhakika wake isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Kwa ajili hii imekuja katika Hadiyth Swahiyh:
“Kila ´amali ya mwanaadamu inalipwa mara kumi. Isipokuwa Swawm tu. Ni yangu na mimi ndio nitailipa. Ameacha matamanio yake, chakula chake na kinywaji chake kwa ajili Yangu.”
Mja anaweza kila siku kujificha na watu na akajifungia nyumbani kwake na akala na kunywa kisha akatoka na kusema kuwa amefunga. Hakuna anayejua hilo isipokuwa Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala). Lakini kitu kinachomzuia kutofanya hivo, ni kwa sababu anajua kuwa Allaah Anamuona na Kumshuhudia. Hichi ni kitu ambacho mtu anasifiwa kwacho. Mazingatio ya yote ni kwamba mtu anajua kuwa Yule Anayeogopwa Swawm ikitumiwa vibaya ndiye Mwenye kuogopwa Swalah, Zakaah, Hajj na matendo mengine yote ya wajibu yakitumiwa vibaya. Yule ambaye Amefaradhisha Swawm ndiye Ambaye Amefaradhisha Swalah. Swalah ndio nguzo kubwa katika Uislamu baada ya kushuhudia kuwa hapana mola anayeabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah. Umuhimu wake ni mkubwa kabisa. Swalah ndio mafungamano ya kila siku kati ya mja na Mola Wake. Allaah Amemfaradhishia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati wa safari ya mbinguni. Ikiwa Muislamu anaonelea kuwa ni dhambi kubwa na nzito kutumia Swawm vibaya, basi ni wajibu atambue kuwa ni dhambi kubwa na nzito zaidi kuitumia Swalah vibaya. Haya ni katika faida na mazingatio makubwa ambayo Muislamu anafaidika nayo katika mwezi wa Swawm.
al-´Ibrah fiy Shahr-is-Swawm
´Abdul-´Muhsin al-´Abbaad
13
www.wanachuoni.com
Ya tatu
Miongoni mwa mambo ambayo yanafungua kifua na kuzifurahisha nyoyo nzuri ni waswalaji kujaa Misikitini katika Ramadhaan. Kitu kinachofungua kifua zaidi na kuzifurahisha nyoyo nzuri zaidi, ni kule kila siku inakuwa ni yenye kujaa. Muislamu anafaidika kupiganisha kudumu siku zote kwa kushikamana na kheri hii ili aweze kuwa miongoni mwa watu saba ambao watapata kivuli cha Allaah siku ambayo hakutokuwa kivuli isipokuwa kivuli Chake. Mmoja wao ni mtu ambaye moyo wake umefungamana na Misikiti, kama ilivyothibiti katika Hadiyth Swahiyh kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
al-´Ibrah fiy Shahr-is-Swawm
´Abdul-´Muhsin al-´Abbaad
14
www.wanachuoni.com
Ya nne
Katika Ramadhaani ni wajibu kujizuia na chakula, kinywaji na vitu vingine vyote vinavyoivunja Swawm. Ama kuhusiana na mambo ya haramu, ni wajibu kujiepusha nayo katika uhai wote. Katika Ramadhaan Muislamu anajizuia na ya halali na ya haramu. Ama kuhusiana na mambo ya haramu, ni wajibu kwake anajizuia nayo katika maisha yote. Masiku ambayo mtu anajizuia na ya halali na haramu yamekwisha, wakati masiku ambayo mtu anajizuia na ya haramu bado ni yenye kuendelea maishani. Swawm kilugha ni mtu kujizuia na kitu. Swawm Kishari´ah ni mtu kujizuia na chakula, kinywaji na mambo yote yenye kuvunja Swawm. Hili huanza pale kunapopambazuka mpaka wakati jua linapozama.
Maana ya Kishari´ah ni sehemu ya maana ya kilugha. Maana ya kilugha inatumiwa kama ya Kishari´ah, zote zina hiyo maana na maana nyinginezo. Miongoni mwa hizo ni kujizuia na ya haramu. Kuzuia macho, ulimi, masikio, mikono, miguu na tupu na yaliyokatazwa inahesabiwa kuwa ni Swawm ya kilugha. Allaah Amemfadhilisha mja kwa neema hizi, Amemkataza vilevile kuzitumia katika njia inayomkasirikisha. Miongoni mwa njia kubwa za kumshukuru Allaah kwa neema hizi, ni yeye kuzitumia kama jinsi Anavyotaka. Nayo ni kwamba mwanaaadamu anatakiwa kuzitumia katika mambo ya wajibu na kujiepusha na yaliyokatazwa.
Kuhusiana na macho, imewekwa kuyatumia katika kutazama yale Aliyohalalisha Allaah na imeharamishwa kutazama ya haramu. Ni kitu ambacho kinatakiwa kuendelea maishani.
Kuhusiana na masikio, imewekwa kusikiliza yaliyoruhusiwa na imeharamishwa kusikiliza yaliyoharamishwa. Kadhalika ni kitu ambacho kinatakiwa kuendelea maishani.
Kuhusiana na ulimi, imewekwa kuutumia katika mambo yote ya wema na imeharamishwa kuutumia katika mambo yote ya haramu. Ni kitu ambacho kinatakiwa kuendelea maishani.
al-´Ibrah fiy Shahr-is-Swawm
´Abdul-´Muhsin al-´Abbaad
15
www.wanachuoni.com
Kuhusiana na mikono, imewekwa Kishari´ah kuitumia katika kuchuma yaliyohalali na imeharamishwa kuchuma yaliyoharamu. Hili ni lazima liendelee maishani.
Kuhusiana na miguu, imewekwa kwenda katika mambo ya kheri na imeharamishwa kwenda katika haramu. Hili pia linatakiwa kuendelea maishani.
Kuhusiana na tupu, imewekwa kuitumia katika njia ya halali na imeharamishwa kuitumia katika njia ya haramu. Ni kitu ambacho kinatakiwa kuendelea maishani.
Wale ambao wanamshukuru Allaah kwa kutumia neema hizi katika njia iliyowekwa, Amewaahidi thawabu kubwa. Kwa upande mwingine Amewatisha wale ambao wanazitumia vibaya. Hakusema tu kwamba matendo kama hayo yanasababisha Ghadhabu za Allaah, bali kwamba yanamridhisha Shaytwaan pia ambaye ni adui wa Allaah na wa waja Wake walio na Ikhlaasw. Allaah Amewatisha kwa adhabu Yake. Amesema kuwa viungo hivi vitaulizwa siku ya Qiyaamah. Allaah (Ta´ala) Amesema: وَلََّ تَ قْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ إِۚنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَ ئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْئُوالَّ
“Na wala usiyafuate (kusema au kufanya) yale usiyokuwa nayo elimu. Hakika masikio na macho na moyo; vyote hivyo daima vitaulizwa (Siku ya Qiyaamah).”13 وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُم بَِِا كَانُوا يَكْسِبُونَ
“Na itatusemesha mikono yao, na itashuhudia miguu yao kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.”14 وَي وَْمَ يُُْشَرُ أَعْدَاءُ اللَّ هِ إِلََ النَّارِ فَ هُمْ يُوزَعُونَ حَ تَّ إِذَا مَا جَاءُوهَا شَهِدَ عَلَيْهِمْ سََْعُهُمْ وَأَبْصَارُهُمْ
وَجُلُودُهُم بَِِا كَانُوا ي عَْمَلُونَ وَقَالُوا لُِْلُودِهِمْ لَِِ شَهِدتُُّّْ عَلَيْ نَا قَۚالُوا أَنطَقَنَا اللَّ هُ الَّذِي أَنطَقَ كُلَّ شَيْءٍ
13 17:36
14 36:65
al-´Ibrah fiy Shahr-is-Swawm
´Abdul-´Muhsin al-´Abbaad
16
www.wanachuoni.com
وَهُوَ خَلَقَكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَإِلَيْهِ ت رُْجَعُونَ
“Na Siku watakayokusanya maadui wa Allaah kwenye Moto, nao wanapangwa safusafu. Mpaka watakapoujia (huo Moto), yatawashuhudia masikio yao, na macho yao, na ngozi zao kwa yale (yote) waliyokuwa wakiyatenda. Na watasema (kuziambia) ngozi zao: “Mbona mnashuhudia dhidi yetu?” (Ngozi zao) Zitasema: “Ametutamkisha Allaah Ambaye Anatamkisha kila kitu, Naye (Ndiye) Aliyekuumbeni mara ya kwanza na Kwake mtarejeshwa.”15
Wakati (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomuamrisha Mu´aadh bin Jabal kuhifadhi ulimi wake, akamuuliza:
“Ee Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), tutahesabiwa kwa yale tunayosema?”
Akasema:
“Mama yako akukose,16 ee Mu´aadh. Ni kitu gani kitachowafanya watu kutupwa Motoni kwa nyuso zao mbele – au kwa mapua yao mbele – ikiwa kama sio ndimi zao?”
Imepokelewa na at-Tirmidhiy.
Amesema vilevile (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Atayenidhamini vilivyo baina ya taya yake na miguu yake; ninamdhamini Pepo.”
15 41:19-21
16 Imaam Ibn-ul-Athiyr (Rahimahu Allaah) amesema:
”Ni kama anaomba ili afe kwa sababu amefanya au amesema kitu cha makosa... Kadhalika inaweza kuwa katika baadhi ya misemo ya waarabu wanaotumia pasina kukusudia hivo. Haikusudiwi Du´aa. Mfano wa hilo ni kama kusema ”Mikono yako ifunikwe na udongo” na ”Allaah Akupige vita”.” (an-Nihaayah (1/214))
al-´Ibrah fiy Shahr-is-Swawm
´Abdul-´Muhsin al-´Abbaad
17
www.wanachuoni.com
Imepokelewa na al-Bukhaariy kutoka katika Hadiyth ya Sahl Sa´d (Radhiya Allaahu ´anhu). Kadhalika at-Tirmidhiy amepokea kutoka katika Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu):
“Yule ambaye Allaah Atamhifadhia vilivyo baina ya käkar yake na miguu yake, ataingia Peponi.”
at-Tirmidhiy ameipa daraja ya Hasan.
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yule anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho aseme mazuri au anyamaze.”
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim kutoka kwa Abu Hurayrah. Wamepokea pia kutoka kwa Abu Muusa (Radhiya Allaahu ´anhu) ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Muislamu ni yule mwenye kuwasalimisha Waislamu kwa ulimi na mikono yake.”
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema pia:
“Mfilisikaji katika Ummah wangu ni yule atayekuja siku ya Qiyaamah na Swalah, Swawm na Zakaah na amemtukana huyu, amemtuhumu huyu, amekula mali ya huyu, amemwaga damu ya huyu na amempiga huyu. Baada ya matendo yake mazuri kwisha na kabla hajahesabiwa, yatachukuliwa mabaya yao na kuwekwa kwake. Kisha atupwe Motoni.”
Ameipokea Muslim.
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Pepo imezungukwa kwa machukizo na Moto umezungukwa kwa matamanio.”
al-´Ibrah fiy Shahr-is-Swawm
´Abdul-´Muhsin al-´Abbaad
18
www.wanachuoni.com
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu).
Allaah Amemuwajibishia mja kuhifadhi ulimi wake, tupu yake, usikizi wake, uoni wake, mikono yake na miguu yake na mambo yote ya haramu. Hii ni Swawm ya kilugha. Inaendelea mpaka Qiyaamah. Inafanywa katika kumtii Allaah ili kuweza kufaulu Radhi Zake na kusalimika na Khasira na Adhabu Zake.
Muislamu anapoona kuwa wakati wa Ramadhaan anajinyima vile Alivyohalalisha Allaah, kwa sababu Allaah Ameviharamisha katika Ramadhaan. Hivyo basi mazingatio ni kwa yeye aone kuwa Allaah Amemharamishia vilivyo vya haramu maishani mwake na kwa ajili hiyo ni wajibu kwake ajiepushe nayo siku zote. Afanye hivo kwa kuogopa adhabu ya Allaah ambayo Ameiandaa kwa yule mwenye kwenda kinyume na maamrisho Yake na kufanya yale Aliyokataza.
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza katika Hadiyth al-Qudsiy kutoka kwa Mola Wake kwamba Amesema mfungaji anapata furaha mara mbili; mara ya kwanza pale anapofungua Swawm na mara ya pili wakati atapokutana na Mola Wake.
Yule anayeuhifadhi ulimi wake kutokana na machafu na kusema uongo, tupu yake kutokana na yale Aliyoharamisha Allaah, mikono yake kuchukua yale Aliyoharamisha Allaah, usikizi wake kutokana na yale Aliyoharamisha kusikia, uoni wake kutokana na yale Aliyoharamisha Allaah kutazama na akatumia viungo hivi katika yale Aliyohalalisha Allaah, akavihifadhi mpaka hapo Allaah Atapomfisha, atakuja kukata Swawm yake kwa aina hii ya Swawm kwa furaha ambayo Allaah Amewaahidi wale wenye kumtii.
Mara ya kwanza wanapokutana na hilo, ni wakati pale ambapo waumini wanapoacha maisha haya na kwenda Aakhirah, jambo ambalo limeelezwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Katika kile kipindi cha mwisho cha dunia hii, Malaika huwajia kwa sura za kung´ara. Wanakuja na sanda na manukato kutoka Peponi. Mbele yao anakuwepo Malaika wa mauti. Aseme: “Ewe nafsi ilio nzuri! Toka katika msamaha na radhi za Allaah.” Hapo ndipo itatoka kama jinsi tone linavyotoka kwenye birika.
al-´Ibrah fiy Shahr-is-Swawm
´Abdul-´Muhsin al-´Abbaad
19
www.wanachuoni.com
Hizi ndio alama nzuri ambazo zinawakumbuka wale wanaopupia kuzifurahisha nafsi zao na kujitahidi kujikwamua na yale yanayopelekea katika maangamivu. Wakati mtu alipomuuliza daktari wa mioyo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu Qiyaamah na kitakuwa lini, alimwelekeza katika kitu ambacho ni muhimu zaidi kuliko Qiyaamah, nacho ni maandalizi na matendo mema. Hakika (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia mtu ambaye aliuliza kuhusu ni lini itakuwa Qiyaamah:
“Umekiandalia nini?”
Hapa anaonesha kuwa mwanaadamu ajiandae katika maisha yake ya duniani. Allaah (Ta´ala) Amesema:
وَتَ زَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْ رَ الزَّادِ التَّ قْوَ ى
17Na jitengenezeeni akiba. Na hakika bora ya akiba ni taqwa.”“
Kila safari inahitajia maandalizi ya sawasawa yenye kutosha na safari ya Aakhirah maandalizi yake ni ucha Mungu, matendo mema na kupita juu ya mfumo uliyonyooka ambao umekuja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
17 02:197
al-´Ibrah fiy Shahr-is-Swawm
´Abdul-´Muhsin al-´Abbaad
20
www.wanachuoni.com
Hitimisho Hitimisho Hitimisho Hitimisho
Nitamalizia muhadhara huu kwa baadhi ya maneno ambayo yanatuhusu sisi ambao Allaah Ametutunukia kwa kuishi katika Daar-ul-Hijrah (al-Madiynah) na mji mkuu wa kwanza wa Waislamu.
Hakika mwezi wa Ramadhaan uliyobarikiwa ni mwezi ambao Allaah Ameutukuza na Kuutofautisha kwa sifa maalum ambazo hazipatikani katika miezi mingine. Siku za karibuni zilizopita, sisi na wengineo katika Ummah wa Kiislamu tumeuaga. Twatarajia sote kuwa miongoni mwa wale ambao wamefuzu kupata Radhi za Mola (Jalla Jallaaluh). Ikiwa huu ni wakati ulio bora na zama tukufu, ni lazima kwetu kujua – na himdi zote ni za Allaah – ya kwamba tunaishi katika mji mtukufu. Allaah Ametujaalia kukutana na Ramadhaan katika muda mtukufu na mji mtukufu. Ikiwa muda mtukufu umekwisha, basi mji mtukufu bado upo. Mbele yetu tuna Msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao ni soko miongoni mwa masoko ya Aakhirah. Ameeleza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Swalah moja katika Msikiti wangu huu ni bora mara elfu kuliko Misikiti mingine yote isipokuwa Msikiti Mtakatifu.”
Hii ni fadhila kubwa kutoka kwa Allaah. Swalah moja katika Msikiti uliyobarikiwa, Msikiti wa Mtume mtukufu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ni bora mara elfu kuliko Misikiti mingine yote isipokuwa Msikiti Mtakatifu.
Watu wanaojishughulisha na biashara za kidunia wanapiganisha kuweza kukutana na misimu yenye kulipa. Wanajiweka katika khatari, wanakata majangwa na wanahama kutoka sehemu kwenda sehemu zingine na biashara zao wanapojua watapata pesa moja katika biashara. Hili ni jambo lisilokuwa na mashaka ndani yake. Sisi katika mji huu mzuri Swalah moja katika Msikiti wa kiumbe bora (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) sio sawa tu na Swalah moja, mbili, tatu, kumi au hata Swalah mia. Bali uhakika wa mambo ni bora mara elfu kuliko Misikiti mingine yote isipokuwa Msikiti Mtakafitu. Ametakasika Allaah! Ni ukubwa na upana ulioje wa fadhila Zake na uzuri Wake? Himdi na sifa zote kamilifu ni Zake Yeye kwa neema Zake.
Kama jinsi neema za Allaah juu yetu katika uzuri ni kubwa, ni juu yetu kutosahau kuwa neema hizi zimetuwekea majukumu makubwa. Kama jinsi
al-´Ibrah fiy Shahr-is-Swawm
´Abdul-´Muhsin al-´Abbaad
21
www.wanachuoni.com
mema yanalipwa kwa ujira uliokuwa mkubwa katika mji huu, basi mtu atambue kuwa dhambi katika mji huu sio kama dhambi katika miji mingine isiyokuwa na ubora. Yule mwenye kutenda maasi akiwa mbali na Haram sio kama mwenye kutenda maasi na yuko Haram. Yule mwenye kutenda dhambi akiwa mashariki na magharibi sio kama mwenye kutenda dhambi akiwa Makkah Takatifu au al-Madiynah al-Munawwarah. Tofauti kati ya hizi mbili ni kubwa. al-Madiynah al-Munawwarah ndio sehemu ilio tukufu zaidi katika ardhi baada ya Makkah Takatifu. Katika ubora al-Madiynah inashika namba mbili baada ya Makkah. Kisha kunakuja Msikiti wa al-Aqswaa´.
Mji huu uliyobarikiwa ndio mji wa Ujumbe. Kutoka katika mji huu ndio nuru ilienea katika kila kona ya dunia. Mji huu ndio markazi, na mji mkuu wa kwanza wa Waislamu katika zama za Mtume, baada ya kuhamia ndani yake. Kadhalika ilikuwa ni mji mkuu wakati wa Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan na baadhi ya wakati wa ´Aliy – Allaah Awawie radhi wote.
Hapa kuna kaburi la Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan na Maswahabah wengine wengi – Allaah Awawie radhi wote.
Katika ardhi hii Jibriyl (´alayhis-Salaam) aliteremka na Wahyi kutoka mbinguni kwa Allaah kumpelekea Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Katika ardhi hii kuna chuo kikuu cha kwanza cha Kiislamu na katika wanafunzi wake ambao ni mabingwa ni Abu Bakr as-Swiddiyq, ´Umar al-Faaruuq, ´Uthmaan Dhuun-Nuurayn na ´Aliy, binamu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wajukuu na Khaliyfah wa nne – Allaah Awawie radhi wote na Maswahabah wengine wote. Ardhi hii ina fadhila na hadhi ya kiuanaadamu baada ya kufa kwa Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Alalahu ´alayhi wa sallam) - Allaah Awawie radhi wote.
Pamoja na kwamba Allaah Ametukirimu kubaki katika mji huu, tuna haki zote za kuweza kujizidishia matendo mema ambayo yatatunufaisha baada ya kufa na tujiepushe na yote yanayopelekea katika Khasira za Allaah (´Azza wa Jalla).
Ninamuomba Allaah (Ta´ala) Atujaalie sote kuwa miongoni mwa wale ambao Anawakubalia Swawm zao na Swalah zao za usiku, Aturuzuku kuishi kwa uzuri na kwa adabu katika nchi hii nzuri na Atujaalie kuwa na mwisho mwema.
al-´Ibrah fiy Shahr-is-Swawm
´Abdul-´Muhsin al-´Abbaad
22
www.wanachuoni.com
Vilevile ninatarajia (Subhaanahu) Awajaalie Waislamu wote kurejea katika Kitabu Chake na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili waweze kufaulu furaha katika maisha haya na Aakhirah.
Hakika Yeye ni Mwenye Kusikia na mwenye kuitikia. Swalah na salaam zimwendeee mja Wake, Mtume Wake, Khaliyli Wake na kiumbe Chake bora Muhammad bin ´Abdillaah, ahli zake, Maswahabah zake na kila mwenye kufuata uongofu wake mpaka siku ya Qiyaamah.

No comments:

Post a Comment